Timu ya Taifa ya mpira wa miguu unaochezwa ufukweni (Beach Soccer), kesho Ijumaa Novemba 9, 2016 inatarajiwa kucheza na Uganda katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika Viwanja vya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo ni maandalizi kwa timu Tanzania na Uganda kujiandaa na michuano ijayo ya kimataifa ndani ya bara la Afrika na ile la  CAF. TFF inatangaza kuwa mchezo huo hautakuwa na kiingilio.
Waamuzi wa mchezo huo watakuwa Jackson Msilombo, Kessy Ngao, Heri Sassii na mtunza muda anatarajiwa kuwa Idd Maganga.
Kocha Mkuu wa timu hiyo Beach Soccer, John Mwansasu anatambia nyota wake 12 wakiwamo makipa Rajab Galla na Khalifa Mgaya.

Mabeki ni Roland Revocatus, Juma Ibrahim, Kashiru Salum na Mohammed Rajab wakati Viungo ni Mwalimu Akida, Ahmada Ali na Samwel John huku washambuliaji wengine wakiwa ni Kassim Kilungo na Talib Ally pamoja na Ally Rabbi ambaye ni Nahodha na Mshambulaji wa timu hiyo.
Hivi karibuni kikosi hiki kilicheza na Ivory Coast katika michezo miwili ya  kuwania nafasi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa yAfrika kwa soka la ufukweni bila mafanikio.

Post a Comment

 
Top