Timu za Taifa za umri
chini ya miaka 23 kwa wanaume na wanawake ambazo hazikuwa na majina sasa
zinaitwa Kilimanjaro Warriors (wanaume) wakati wanawake ni Kilimanjaro
Starlets.
Uteuzi wa majina hayo umefanywa na
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika
kikao chake kilichofanyika jana (Desemba 17, 2016) jijini Dar es
Salaam.
Timu hizo ambazo ni maalumu kwa ajili
ya michuano ya Olimpiki zitaanza maandalizi yake Januari mwakani, na
wengi wa wachezaji watakaounda timu hizo zinazojiandaa kwa ajili ya
michuano ya Olimpiki itakayofanyika Tokyo, Japan mwaka 2020 watatoka
katika timu za sasa za wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 (U20).
Mechi za mchujo (qualifiers) kwa ajili ya michuano ya Olimpiki ya 2020 zitaanza mapema mwaka 2019.
Post a Comment