KOCHA Mkuu
wa Yanga, George Lwandamina amefunguka kuwa kazi kubwa aliyonayo sasa ni
kuhakikisha anaendelea kuifanya kazi aliyoachiwa na mtangulizi wake, Hans van Der
Pluijm ya kupigania ubingwa na kazi hiyo ataanza nayo kesho Jumamosi katika
mechi dhidi ya JKT Ruvu.
Lwandamina
anatarajiwa kuwa kwenye benchi kwa mara ya kwanza katika mechi ya mashindano
akiiongoza Yanga katika mchezo huo wa raundi ya pili wa Ligi Kuu Bara kwenye
Uwanja wa Uhuru jijini Dar.
Kocha
huyo amesema kuwa licha ya ugeni wake katika soka la Tanzania lakini kwa msaada
anaopata kutoka kwa mtangulizi wake, Pluijm ambaye ni Mkurugenzi wa Ufundi wa
Yanga kwa sasa, amedai kuwa ameshawajua wapinzani wake na anaamini ataanza kwa
ushindi.
“Yanga
ni mabingwa watetezi, kazi yangu ni kuhakikishia tunautetea, nalifanyia kazi
hilo, tuna wachezaji wazuri wanaoweza kutimiza kazi hiyo.
“Nimeshaambiwa
siri zao (JKT), tuna nafasi kubwa ya kushinda,” alisema Lwandamina.
Aidha, Lwandamina amesema Yanga
ina malengo yake kadhaa na mawili makubwa ni ubingwa wa Bara na kufanya vizuri
katika michuano ya kimataifa, lakini akasema mpaka sasa ameshafanya maandalizi
mazuri lakini bado kuna vitu vya kuweka sawa na anaamini baada ya muda kikosi
kitakaa sawa.
Post a Comment