KOCHA Mkuu wa Yanga Mzambia, George Lwandamina
amembadilishia majukumu mshambuliaji wake, Juma Mahadhi kwenye kikosi hicho.
Hiyo, ikiwa ni wiki moja tangu kocha huyo aanze kukinoa
kikosi hicho kinachojiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara utakaoanza
Jumamosi ijayo.
Kocha huyo, hivi sasa yupo katika mipango thabiti ya
kukiboresha kikosi chake ili kuhakikisha anapata wachezaji 11 watakaokuwa
wanaanza.
Mzambia huyo, kwenye mechi ya wikiendi iliyopita na JKU
alimchezesha Mahadhi namba nane, nafasi inayochezwa kwenye timu hiyo na
Mnyarwanda, Haruna Niyonzima na Mzimbabwe, Thaban Kamusoko.
Katika mechi hiyo iliyomalizika kwa Yanga kufungwa mabao
2-0 yote yakifungwa kipindi cha kwanza, Mahadhi alionyesha umahiri wa
kuchezesha timu na kukaa na mpira huku akipiga pasi safi kwa wachezaji wenzake.
Mshambuliaji huyo, alicheza katika nafasi hiyo kwa dakika
45 za mchezo huo, kabla ya kipindi cha kutolewa na nafasi yake ikachukuliwa na
Kamusoko.
Akizungumzia hilo, Lwandamina alisema: "Hivi sasa
ninatengeneza kikosi cha kwanza nitakachokitumia kwenye mzunguko wa pili wa
ligi kuu, hivyo ni lazima nimjaribu kila mchezaji ili nione uwezo wake.”
Post a Comment