HAKIKA
unaweza kushangazwa na namna Simba inavyohaha kuwabakiza vijana iliowalea na
taarifa zinasema kijana aliyepewa unahodha, Jonas Mkude amewazimia simu
viongozi wa klabu hiyo.
Habari
za uhakika zinasema, Simba wamekuwa wakihaha kumpata Mkude ili kumalizana naye
katika suala la usajili, lakini yeye alikuwa amezima simu tangu Jumatatu.
“Kweli
Mkude alizima simu kabisa baada ya kuwa tumefanya naye majadiliano kwa mara ya
kwanza. Kukawa hakuna mwafaka sahihi, wakati tunasubiri arudi kumalizana naye,
akazima simu.
“Tulimtafuta
kwa siku mbili, mwisho tukawaambia Meneja Mussa Mgosi na Mratibu, Abbas Ally
kumtafuta. Nao wakafanya hivyo bila ya mafanikio na mwisho tumeamua kukaa kimya
na kusubiri,” chanzo cha habari kutoka ndani ya Simba kilieleza.
“Sasa
kama anataka kusaini sawa, au tumesikia kuna mtu kamshawishi asisaini ili
akacheze Afrika Kusini sawa. Tunajua namna ya kulifanyia kazi hili na kupata
jibu. Tumechoka kufanywa kama watoto.”
Imeelezwa,
ili kuongeza mkataba Mkude alikuwa akitaka kupewa Sh milioni 80, baadaye
akashuka hadi 60 wakati Simba walikuwa wameishia 40, wakapanda hadi 50 na Mkude
ndiyo akaamua kuzima simu.
Wiki
hii mwanzoni, Mkude aliliambia gazeti hili atakwenda kusaini Yanga badala ya
Simba kama hali ya kutofikia mwafaka itaendelea.
Lakini
siku chache baadaye, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga naye akatoa
kauli yake kwamba hawana mpango na Mkude na wanaangalia mbali zaidi kwa kusaka
viungo ‘wakata umeme’ wenye uzoefu kwa ajili ya michuano ya kimataifa na
inaelezwa hiyo inaweza ikawa sababu ya kumtia hofu Mkude na huenda akaanza
kuwatafuta viongozi wa Simba, ili wamalizane.
Inaripotiwa
kuwa juzi na jana Mkude alikuwa mmoja wa wachezaji wa Simba walioshiriki katika
mazoezi ya timu hiyo kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi jijini Dar.
Post a Comment