ARSENAL inajipanga kwa vita na Everton
katika kuwania saini ya beki wa kati wa Swansea, Ashley Williams, ambaye dau
lake linatajwa kuwa pauni milioni 10. Arsenal pia imetajwa pia kutenga pauni
milioni 15 kwa ajili ya kumsaini beki wa West Brom, Jonny Evans, 28.
Sunderland
KOCHA mpya wa Sunderland, David Moyes
anataka kuwasjaili nyota aliokuwa nao Man United, kiungo Marouane Fellaini na Adnan
Januzaj.
Roma
ROMA imeongeza kasi ya kutaka kupata
saini ya beki wa Manchester United, Matteo Darmian baada ya walinzi wake, Mario
Rui na Antonio Rudiger kuumia hivi karibuni.
West Ham
WEST Ham inajipanga kutoa ofa ya
pauni milioni 20 ili ipate ridhaa ya kumsajili mshambuliaji wa Swansea City,
Andre Ayew, baada ya ile ya kwanza ya pauni milioni 16 kukataliwa.
Man City
MANCHESTER City inakaribia
kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Schalke, Leroy Sane baada ya kukubali
kutoa dau ya pauni milioni 31.2.
Chelsea
MENEJA wa Chelsea, Antonio Conte anaamini
klabu yake itamsajili tena aliyekuwa mshambuliaji wa kikosi hicho, Romelu
Lukaku, 23, kutoka Everton. Blues wamepanga kutoa ofa ya pauni milioni 60.
Arsenal
ARSENAL wamepanga kumtengea pauni
milioni 50 straika wa Inter Milan, Mauro Icardi, 23, ikiwa watashindwa
kukamilisha dili la mshambuliaji wa Lyon, Alexandre Lacazette, 25.
Galatasaray
KIUNGO wa Liverpool, Lucas Leiva, 29,
anatarajiwa kukamilisha dili la kujiunga na Galatasaray ya Uturuki kwa dau la
pauni milioni 2.3 wiki hii.
Man United
KOCHA wa Manchester United, Jose
Mourinho anataka kumsajili beki wa kati mwenye uzoefu kikosini humo ili
kuongeza nguvu msimu ujao. Pia beki wa Chelsea, Baba Rahman, 22, anatarajiwa
kujiunga na Schalke kwa mkopo wa muda mrefu.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.