Mwenyekiti wa zamani wa Simba Ismail Aden Rage, amemtaka
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe kumuomba radhi
ndani ya siku tatu.
"Nadhani mtu mwendawazimu tu anaweza kufanya hivyo, mke
wangu hana hata akaunti. Nimeshamuambia wakili wangu amshughulikie, aniombe
radhi ndani ya siku sana. La sivyo suala hili litaenda mahakamani,"
alisema Rage.
"Sasa hivi tunazungumzia suala la fedha za Okwi na si
fedha za Samatta," aliongeza Rage.
Rage amemtaka Hans Poppe kumuomba radhi kutokana na kauli
yake kwamba fedha za malipo ya Mbwana Samatta kutoka TP Mazembe, zilipitia
kwenye akaunti ya mkewe.
Hans Poppe alisema hayo jana wakati akifafanua kuhusiana na
suala lililo Takukuru baada ya Rais wa Simba, Evans Aveva kushikiliwa,
kuhojiwa. Baadaye wakahojiwa wajumbe wa kamati ya utendaji.
Rage amezieleza taarifa hizo za Hans Poppe kuwa ni uzushi
usiokuwa na maana, hivyo anasisitiza anatoa siku tatu za kuombwa radhi.
Salehjembe
Post a Comment