WANACHAMA wa Yanga wamekubali kumkodisha klabu hiyo
Mwenyekiti wao, Yusuf Manji kwa miaka 10 kuanzia leo.
Uamuzi huo umefikiwa katika Mkutano Mkuu wa dharula
uliofanyika leo ukumbi wa Diamond jubilee, Dar es Salaam.
Manji ameomba apewe klabu kwa miaka 10 na katika kipindi
hicho atakuwa anachukua asilimia 75 ya mapato ya timu, huku asilimia 25 ikibaki
kwa wanachama.
Na katika kipindi hicho cha miaka 10, timu ya soka na nembo
ya klabu zote zitakuwa chini ya Manji. Aidha, Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la
klabu, Francis Kifukwe alisema baada ya wanachama kuridhia mpango huo, wao
wanampa pia ridhaa hiyo Manji
Mkutano wa Yanga unaendelea hivi sasa Diamond Jubilee na
awali wanachama watatu wa klabu hiyo, Ayoub Nyenzi, Salum Mkemi na Hashim
Abdallah walifukuzwa.
Manji aliwaambia wanachama hayuko tayari kufanya kazi na
Wajumbe hao wa Kamati ya Utendaji na akaomba wanachama wanaowataka wajitokeze
kupiga kura, lakini hakuna aliyeinuka.
Baada ya kurudia kuita mara tatu, Hashim pekee kati ya watatu
hao ambaye alikuwepo mkutanoni ukumbi wa Diamond Jubilee, akainuka na kuondoka.
Mwanachama mwingine, Siza Lyimo ambaye Manji alitaka aondoke,
yeye aliomba msamaha na wanachama wakamsamehe na Mwenyekiti huyo akabariki
msamaha huo.
Mkemi na Nyenzi hawakutokea kwenye Mkutano huo.
Binzubery


Post a Comment