Taarifa zilizotufikia zinaeleza kwamba Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva ameachiwa baada ya kushikiliwa toka jana na Taasisi ya kupambana na kuzuia Rushwa (TAKUKURU).
Jambo kubwa lililosababisha Aveva kutiwa lupango linaelezwa kuwa ni kuhamisha fedha za Usajili wa Emmanuel Okwi (Dola laki tatu) zilizoingia kwenye akaunti ya Simba na kuingiza kwenye akaunti yake kwa lengo la kukwepa kodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Hata hivyo malipo hayo ya fedha Shilingi milioni 600 ni malipo ya ununuzi wa mshambuliaji Emmanuel Okwi ambazo Simba ilimuuza katika klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia.
Inadaiwa uongozi uliamua kuzificha ili waweze kujenga uwanja wao wa Bunju ambao tayari walianza kuujenga.
Chanzo: MPENJA SPORTS

Post a Comment

 
Top