KUELEKEA msimu ujao wa Ligi
Kuu Bara, Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog, raia wa Cameroon, tayari
ametengeneza vikosi viwili ambavyo ukiviona vyote ni vya ushindani.
Kikosi ambacho kinaonekana kuwa ni cha kwanza, kinaundwa
na Vincent Angban, Besala Bokungu, Mohammed Hussein ‘Zimbwe Jr’, Juuko Murshid,
Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Mzamiru Yasin, Fredric Blagnon,
Ibrahim Ajib na Jamal Mnyate ambacho kinatumia mfumo wa 4-5-1.
Cha pili ni, Peter Manyika, Hamad Juma, Abdi Banda,
Novaty Lufunga, Emmanuel Semwanza, Said Ndemla, Peter Mwalyanzi, Mohammed
Ibrahim, Danny Lyanga, Mousa Ndusha na Mwinyi Kazimoto, hiki kinatumia mfumo wa
4-3-3.
Omog alisema kuwa:
“Katika kutengeneza timu ya ushindani ni lazima uwe na wachezaji wengi ambao
ukiwaanzisha kwenye mechi, unajua kabisa yupo wa kuingia baadaye na kubadili
mchezo.
“Ukiangalia kikosi changu hiki nakiona kwa mtindo huo na
hii inanipa wakati mzuri wa kuijenga Simba imara zaidi ya kuja kushindania
mataji.”



Post a Comment