STRAIKA mpya wa Simba, Laudit Mavugo amefunguka kwa mara
ya kwanza sababu iliyomfanya ashindwe kutua mapema kwenye klabu hiyo.
Hivi karibuni Rais wa Simba, Evans Aveva alisema
walikuwa wakimtafuta mara kwa mara mchezaji huyo ili aende kusaini kandarasi
licha ya kulipwa chake lakini alikuwa hapatikani kwenye simu yake.
Akizungumza na spotiripotablog, Mavugo alisema: “Katika
hilo viongozi wa Simba hawapaswi kulaumiwa ila mimi ndiye niliyekuwa na makosa
lakini siwezi kusema ni makosa gani hayo.
“Nachoweza kusema ni kwamba nashukuru Mungu safari hii
nimefanikiwa kuja na nitaitumikia Simba kwa moyo wangu wote kwa sababu
ninaipenda tangu nikiwa mdogo, mambo yaliyopita naomba tuyaache, tugange
yajayo.”
Post a Comment