MCHEZAJI wa Mchezo wa Upondo raia wa Japan, Pole Vault Hiroki Ogita amesema ameshangazwa baada ya ripoti kusema kuwa sehemu yake nyeti ilimzuia kusonge mbele katika michezo ya Olimpiki ya Rio de Janeiro.
Kanda ya video ya mwanariadha huyo inayoonyesha kitu kutoka mbele kwa mwanamichezo huyo kikigonga mbele ya ufito ilisambaa haraka katika mitandao ya kijamii.

Lakini kabla ya eneo hilo kugusa mti huo ambao unatumika kwa ajili ya kurukia, miguu yake ilikuwa tayari imeugonga ufito huo huku mikono yake nayo ikimalizia kuuangusha mti huo.
''Sikudhani kwamba vyombo vya habari vya kigeni vingeweza kunidhalilisha hivi. 'Si swala geni iwapo ni ukweli lakini ni swala la kuhuzunisha kwa kulifanyia mazaha jambo kama hili.” aliandika mwanariadha huyo wa miaka 28 katika mtandao wake wa Twitter.
Mkufunzi wa mchezo huo, David Yeo kutoka Singapore, amesema kuwa tayari alikuwa ameugonga ufito huo kupitia mwili wake
''Nadhani ni kuanguka kwa ufito huo ndio kuligusa eneo hilo nyeti kwa bahati mbaya''.
Bwana Ogita hata hivyo aliuruka ufito huo katika jaribio lake la pili lakini akashindwa kuendelea baada ya kuruka urefu wa mita 5.45 pekee ukiwa ni mruko wake wa mwisho.

Post a Comment

 
Top