WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa ngazi ya Klabu, Yanga leo wamerejesha matumaini ya kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mo Bejaia.

Bao pekee la Yanga lilifungwa na Amissi Tambwe raia wa Burundi katika dakika ya nne ya mchezo huo uliokuwa wa kuvutia huku ukishuhidiwa Yanga ikikosa mabao mengi ya wazi kupitia kwa washambuliaji wake.

Kabla ya mchezo wa leo dhidi ya Waarabu hao, Yanga ilikuwa na alama moja huku ikiwa imeshuka dimbani mara nne. Pointi hiyo moja waliipata katika sare dhidi ya Medeama ya Ghana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ambapo walifungana bao 1-1.




Kwa ushindi huu wa leo, Yanga sasa wamefikisha alama nne huku wakiwa bado mkiani lakini sasa wanatakiwa kuiombea TP Mazembe iifunge Medema ambayo itakuwa kwenye uwanja wake wa nyumbani hapo kesho.

Lakini huku ikiombea Medema wafungwe Yanga na yenyewe itatakiwa kuifunga Mazembe kwenye mchezo wake wa mwisho utakaopigwa Agosti 23 huko Lubumbashi DR Congo huku ikiombea sare mechi ya Mo Bejaia na Medeama itakayopigwa siku hiyohiyo huko Algeria.

Post a Comment

 
Top