Yanga na Azam FC zinatarajiwa kukutana leo Jumatano katika mechi ya Ngao ya Hisani ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2016/17, tayari kila upande unaonekana kuwa tayari.
Yanga ambao
upande wa uongozi kwa sasa hakujatulia kutokana na taarifa za mwenyekiti wao,
Yusuf Manji kutaka kujiuzulu nafasi hiyo, kikosi chao kipo kwenye mazoezi
katika Uwanja wa Gymkhan jijini Dar es Salaam wakati Azam FC wao wapo kwenye
Uwanja wao wa Azam Complex nje kidogo ya Dar es Salaam.
Mchezo huu
pia utakuwa wa kwanza wa ushindani kwa benchi zima la Azam likiongozwa na Kocha
Mkuu, Zeben Hernandez ambaye ni raia wa Hispania.
Post a Comment