MECHI ya Ngao ya Jamii itakayowakutanisha Yanga na Azam, inatarajiwa kuamuliwa na mwamuzi aliyetwaa tuzo katika msimu uliopita wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Ngole Mwangole.
Timu hizo zitakutana tena keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, baada ya msimu uliopita ambapo Yanga walifanikiwa kutwaa ngao hiyo kwa mikwaju ya penalti 8-7 kufuatia kutoka suluhu ndani ya dakika 90.
Mwangole ambaye ni mwamuzi mwenye beji ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), atasaidiwa na Joseph Bulali kutoka Tanga na Frank Komba wa Dar es Salaam.
Akizungumza na BINGWA jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi wa TFF, Salum Chama, alisema kamisaa wa mchezo atakuwa Peter Temu kutoka Arusha.
Chama alisema baada ya mechi hiyo ya ufunguzi, Ligi Kuu itaanza Agosti 20 mwaka huu, katika viwanja mbalimbali nchini.

Post a Comment

 
Top