Mapema leo kuliibuka taarifa kuwa Yanga inaweza kumpoteza
mwenyekiti wake Yusuf Manji ambaye inadaiwa kuwa anataka kutangaza kujiuzulu
nafasi hiyo na kusitisha kusudio lake la kuichukua na kuendesha kibiashara timu
ya Yanga na nembo yake.
Habari hiyo imekuwa ikisambaa kwa kasi katika mitandao
mbalimbali na mmoja wa viongozi wa Yanga alikiri kuwa suala hilo lipo.
Licha ya taarifa hizo kusambaa kwa kasi bado hakuna taarifa
rasmi kuwa kiongozi huyo amechukua uamuzi huo zaidi ya tetesi.
Kwa mujibu wa mtandao wa salehjembe.blogspot.com, Manji
amenuukuliwa akisema kuwa anataka aachwe na hataki kujibu hoja hiyo kama kweli
amejiuzulu au la.
Baada ya taarifa hiyo kuendea Wanayanga wengi wamekuwa na
maoni tofauti wapo wanaolalamika kuwa Manji ni mkombozi wao hasa katika masuala
ya fedha na wengine wanadai anaweza kuondoka tu kwa kuwa msaada wake umefikia
ukomo. Mjadala unaendelea.
Post a Comment