AKICHEZA
mchezo wake wa kwanza wa ushindani tangu asajiliwe kwenye Klabu ya West Ham,
mshambuliaji Andre Ayew ameanza kwa majanga baada ya kuumia na kudaiwa kuwa
atakuwa nje kwa muda wa miezi minne.
Ayewe
aliumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu England, dhidi ya Chelsea Jumatatu ya wiki
hii na kuchapwa mabao 2-1.
Ayew ambaye ni
raia wa Ghana alicheza kwa dakika 30 tu kabla ya kupata majeraha ya paja na
kulazimika kutolewa huku nafasi yake ikichukuliwa na Gokhan Tore.
Kwa mujibu
wa Mkuu wa Idara ya masuala ya kitabibu wa West Ham, Stijn Vandenbroucke, Ayew aliyejiunga
na Hammers msimu huu kwa dau la pauni milioni 20.0 kutoka Swansea, analazimika
kuwa nje kwa kipindi hicho kutokana na jeraha lake kuhitaji kufanyiwa upasuaji
ili kupatiwa ufumbuzi.
Post a Comment