NYOTA wa
Kimataifa wa Argentina na klabu ya Neuva Chicago Rodrigo Federico Espindola
amefariki dunia leo baada ya kupigwa risasi tumboni na watu wanaodhaniwa kuwa
ni majambazi.
Rodrigo
mwenye miaka 26 amekutwa na mkasa huo mbaya nje kidogo ya mji wa nyumbani kwao
wa Monte Grande huko Buenos Aires wakati akijaribu kuzuia tukio la uporaji
lililokuwa likiwahusisha mke na mtoto wake mdogo wa kiume.
Taarifa
zaidi zinasema Rodrigo aliyekuwa akicheza nafasi ya ulinzi amefariki muda mfupi
baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Santa Maria kwa ajili ya kupatiwa
matibabu ya jeraha lake.
Post a Comment