MASTAA wa muziki Beyonce Knowles, 34, na mumewe Jay Z, 46, wameonekana kuwa bado wana mapenzi mazito mioyoni mwao kufuatia kuonekana wakiwa pamoja na binti yao, Blue Ivy wakipata chakula cha usiku mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mapema wiki hiyohiyo kulikuwa na tamasha linalofanyika kila mwaka la maonyesho ya urembo liitwalo Met Gala, ambapo Beyonce pekee alihudhuria hivyo kujenga picha kuwa wawili hao huenda bado wapo kwenye mfarakano.
Beyonce na Jay Z wamekuwa wakiripotiwa kuwa hawapo sawa kwenye maisha yao ya ndoa huku watu wakifika mbali zaidi na kudai album mpya ya mwanadada huyo, Lemonade  ni dongo kwa mumewe.

Hata hivyo mtandao mmoja wa habari za burudani umedai kuwa chanzo chao kiliwaona wawili hao wakiwa pamoja kwenye Mgahawa wa Mamo huko New York wakipata chakula cha usiku huku wakishikana mikono mara kwa mara kuonyesha kuwa wapo pamoja.


Post a Comment

 
Top