WACHEZAJI WA AZAM FC
Na Ariana Yohana
Timu ya Azam FC ya Dar es Salaam, imenyang'anywa
ushindi wa pointi tatu na mabao matatu uliyoupata katika mechi Na. 156
ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City.
Kitendo hicho ni kinyume na Kanuni ya 37(4) ya Ligi Kuu Toleo la 2015 inayoelekeza kuwa mchezaji atakayeonywa kwa kadi ya njano katika michezo mitatu hataruhusiwa kucheza mchezo unaofuata wa timu yake. Hivyo kwenda kinyume na Kanuni husika.
Pia kwa kuzingatia Kanuni ya 14(37) ya Ligi Kuu Toleo la 2015, timu ya Mbeya City imepewa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu.
Kadhalika Bodi ya Ligi imelionya Benchi la Ufundi la timu hiyo kuongeza umakini katika utunzaji wa kumbukumbu za kadi za wachezaji wake. Pia imezikaribisha timu zote wakati wowote kuomba kumbukumbu zozote kila zinapozihitajika.
Post a Comment