ANDY CARROLL
atabaki na kumbukumbu zake milele baada ya kuwa na msimu mzuri akiwa
anaitumikia West Ham.
Lakini
straika huyo wa zamani wa Liverpool kama angelemaa, mkewe angeweza kuuza mpira
alioupata baada ya kufunga ‘hat- trick’ dhidi ya Arsenal mwezi uliopita.
Carroll
alisema: “Binafsi kumbukumbu yangu bora
zaidi msimu huu ni hat-trick dhidi ya Arsenal. Nilipata mpira tuliochezea mechi
hiyo na kuuweka katika kabati la kioo, ukiwa salama umefungiwa katika kabati
nyumbani na hakuna anayeweza kuugusa.
“Mke wangu
aliniuliza siku moja kama anaweza
kufanya biashara kwa kuutangaza kwenye mtandao na kuuza. Lilikuwa moja kati ya maswali ya mzaa lakini unajua
kwamba kama ningesema ndio, ungekuwa
umeondoka sasa. Lakini mpira huu unamaanisha kila kitu kwangu.
“UnasaIdia
kuonesha kwamba nimepitia magumu nimepitia njia ya kutisha ya majeraha na
nimerudi tena kwenye kupachika mabao. Nimefikia
hatua hiyo baada ya kutoka kwenye majeraha ambayo nimechoka kuyazungumzia.
Pindi unapoumia kifundo cha mguu na kutundika viatu vyako nyumbani unaanza
kuhisi labda kuna mtu yupo kwa ajili yako,” alisema Carroll.
Post a Comment