Ni dakika 270 tu zimebaki kabla ya timu ya soka ya Yanga SC
kushinda ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara na kufuzu kwa hatua ya makundi ya
michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu. Kikosi hicho kinahitaji
pointi tatu tu dhidi ya Mbeya City FC ili kushinda ubingwa wao wa 25 wa VPL,
kisha watalazimika kupambana kufa na kupona na kuwashinda Waangola, Esperanca
katika mipambano miwili ya ‘play off’ ili kufuzu kwa 8 bora ya michuano ya CAF.
Kama kawaida mtandao wa www.shaffihdauda.co.tz umefanya
mahojiano na mlinzi namba mbili wa timu ya Yanga, Juma Abdul Jaffar kuhusu
nafasi yao katika VPL na michuano ya CAF.
Hadi sasa Juma amefanikiwa kufunga jumla ya magoli matano
(5) na kusaidia kupatika kwa magoli 12 (ameasissts magoli 12) katika michezo ya
ligi kuu pekee. Michezo mingine minne katika michuano ya ligi ya mabingwa
Afrika ambako Yanga walitolewa hatua ya 16 na Al Ahly ya Misri, mlinzi huyo
mwenye tabia ya kupandisha mashambulizi na kwenda mbele amehusika katika magoli
matatu ya timu yake.
Amefunga mara moja na kuasisst magoli mawili kwa maana hiyo
Juma Abdul hadi wakati huu tayari amehusika kikamilifu katika magoli 20 ya timu
yake. Ni mafanikio mengine ya aina yake kwa mlinzi huyu namba 2.
www.shaffihdauda.com: Hongera sana kwa msimu mzuri uliokuwa
nao, unakiweka kiwango chako cha msimu huu kwenye nafasi gani kwa kutofautisha
na misimu yako mitatu ya mwanzo hapo Yanga?
Juma Abdul: Nakiweka kwenye kiwango cha kimataifa sasa maana
sidhani kama kuna mchezaji anapokuwa kwenye kiwango kizuri akawa anafikiria
kurudi chini, anawaza kuongeza mara mbili ili awezefika anapopataka.
www.shaffihdauda.com: Msimu huu VPL umecheza game ngapi na
magoli mangapi umefunga, unakumbuka na assists zilizozaa magoli?
Juma Abdul: Sikumbuki nimecheza mechi ngapi lakini kama
asilimia tisini (90%) na kufunga magoli
matano hadi sasa. Toka ligi imeanza assists kumi na mbili (12) ukiacha mechi
nyingine hizo katika ligi tu.
Mechi za kimataifa nimecheza nne na kufunga goli moja na ku-
assists mara mbili mechi dhidi ya Joachim (kwao) tulishinda 1-0, nili assist
game ya marudiano sikucheza lakini nilipata kadi ya njano moja ikafuata, ya APR
kwao nikafunga goli nikapata kadi ya njano marudiano home sikucheza ikaja ya Al Ahly home tulitoka 1-0 siku-assist kwao
nime-assist kwa hiyo assists jumla ni
mbili na kufunga goli moja.
www.shaffihdauda.com: Asante sana. Kama mtashinda game ya
VPL (Mbeya City) mtashinda ubingwa, pia mna mechi mbili (home/away) dhidi ya
Waangola Esperanca, dakika 270 zijazo zina maana gani kwenu kama timu, wewe
kama mchezaji?
Juma Abdul: Tukiwa kama timu tunahitaji kujitoa zaidi ili
kuhakikisha tunapata hizo pointi tatu muhimu ili tuweze kutetea ubingwa wetu na
nikiwa kama mchezaji napaswa kujitambua ili kuweza kulinda kiwango changu
‘istoshe’ ili uonekane kwenye mashindano
ambayo tunacheza haya ya kimataifa hii ndiyo nafasi ya sisi kujiuza mbele kwa
hiyo tunaitaji kufanya jitihada kubwa ili tuweze kuwatoa hawa Waangola ili
tufuzu kwenye hatua ya makundi.
www.shaffihdauda.com: Unaichukulia Esperanca ambao ni
wapinzani wenu wajao?
Juma Abdul: Siwezi kusema chochete juu ya hiyo timu kwa
sababu hatujawahi kukutana nayo wala kuwaona wanavyo cheza kikubwa sisi tunachopaswa
ni kupambana ili kuhakikisha hapa nyumbani tunashinda ushindi ulio mzuri.
www.shaffihdauda.com: Kucheza michezo mikubwa ya mtoano
kumeongeza presha kwako?
Juma Abdul; Hapana, zaidi imeniongezea kujiamini na
kujitambua kuwa naweza kucheza sehemu yoyote duniani na kufanya vizuri.
www.shaffihdauda.com: Mlicheza na Al Ahly game ya kwanza
mkiwa nyumbani na kupata sare ya 1-1, kisha mkapoteza 2-1 ugenini. Dhidi ya
Esperanca pia mtaanza nyumbani na ile ya marudiano mtacheza huko Angola.
Umekuwa ukiwaza kuwa ni afadhali mngemalizia nyumbani? Kutokana na kwamba 2014
mlitolewa baada ya matokeo mabaya ya ugenini na ilikuwa hivyo tena dhidi ya
Etoile du Saleh mwaka jana
Juma Abdul:Yeah,
unajua unapoanza ugenini unajua unajipanga vipi kuhakikisha unapata hata
suluhu au ushindi ukija home unajipanga upya kuweza kuwatoa wapinzani.
Kwanza, unakuwa na sapoti kubwa ya
mashabiki wenu lakini kwa sisi Yanga huwa naona bora tuanze home kisha
tumalizie away sababu tunachezaga vizuri zaidi ugenini kwa kuwa kunakuwa hakuna presha ya mashabiki
wetu, hapa nyumbani kunakuwa na presha kubwa sana ya mashabiki wetu sababu
wanahitaji ushindi waharaka.
www.shaffihdauda.com: Unadhani kuwasoma wapinzani wako
kimchezo kabla ya kukutana nao inasaidia?
Juma Abdul: Ndiyo inasaidia sana sababu unapata nafasi ya
kumjua kabisa mpinzani anatumia silaha ipi kwa hiyo ukishajua unajipanga
kumkabili na wewe na silaha zako.
www.shaffihdauda.com: Unadhani Yanga ipo juu kwa sasa na
inatakiwa kucheza 8 bora ya CAF?
Juma Abdul: Ndiyo ukizungumzi Yanga kwa sasa ipo vizuri kwa maana ina kikosi bora kwa hiyo wana kila
sababu yakuvuka makundi CAF.
www.shaffihdauda.co: Endapo Yanga itafanikiwa kupenya katika
hatua hii ya mtoano na kufuzu kwa makundi, Je, inaweza kuwa miongozi mwa timu
zinazoweza kufanya maajabu katika michuano hiyo?
Juma Abdul: Mimi labda niseme kitu kimoja kama Yanga
tutafanikiwa kupita hatua hii na kufuzu hatua ya makundi, basi naimani tunaweza
kuushangaza ulimwengu kwani yote yanawezekena kikubwa kumuomba Mungu atujalie
pumzi na kutokuwepo na majeruhi.
www.shaffihdauda.co: Nafahamu tangu upo Toto Africans
2011/12 ambao ulikuwa msimu wako wa kwanza kucheza VPL ulikuwa ukifunga sana,
pia ulikuwa ukifunga wakati ukiichezea Mtibwa Sugar siku zote umekuwa ukifunga
magoli muhimu au kutengeneza nafasi kwa wenzako mkiwa kwenye nyakati ngumu za
mechi, unawezaje kufanya hivyo?
Juma Abdul: Ni nikipaji changu au cha mchezaji mwenyewe na
ufanisi wake wa kazi pindi awapo mazoezini na hata kwenye mechi kwa hiyo mimi
ukiangalia swala la kufunga sijaanzia Yanga tokea nyuma nilipotoka nilikuwa
nafunga na ku-assists.
www.shaffihdauda.co: Ni mabadiliko gani uliyoyafanya hadi
kufikia kuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza kwa zaidi ya miezi 12 sasa?
Ukizingatia wakati fulani ulikuwa na majeraha ya mara kwa mara
Juma Abdul: Hakuna mabadiliko yoyote niliyo yafanya zaidi
yakuongeza kufanya mazoezi binafsi hilo ndiyo kubwa na swala la majeraha
inatokea tu kwa mchezaji tunaona hata Ulaya mtu kama Sturridge kila mara
anapata majeraha.
www.shaffihdauda.co: Unajisikiaje kucheza katika kiwango cha
juu msimu huu?
Juma Abdul: Najisikia vizuri sana sababu naona kabisa ndoto zangu nilizokuwa naziwaza
zinaendea kutimia.
www.shaffihdauda.co: Uliwahi kupoteza matumaini ya kucheza
mbele ya Shadrack Nsajigwa au Mbuyu Twite?
Juma Abdul: Sijawahi kupoteza matumaini hayo sababu mimi mwenyewe nilikuwa naamini naweza kwa
hiyo nilikuwa nasubiria muda tu japokuwa hao watu wote uliyowataja nilikuwa
napenda sana uchezaji wao na kujituma kwao kwa hiyo mimi nilikuwa nakopi vitu vyao kisha navifanyia kazi
ndiyomaana unaona mpaka sasa nipo kwenye first aleven.
www.shaffihdauda.co: Unamalizika mkataba na Yanga, je, kuna
ofa umepata mahala?
Juma Abdul: Nyingi sana lakini siwezi kuziweka wazi coz mimi
bado mchezaji wa Yanga.
www.shaffihdauda.co: Vizuri, za nje ya nchi zinaweza kufika
ngapi? kuna habari kwamba tayari umezungumza na timu yako ya sasa na utasaini
mkataba mpya hapo imekaaje hii.
Juma Abdul: Hahahahahaaa, huwezi kusema ngapi lakini
itajulikana kila kitu kikiwa tayari kwa kuwa mimi bado mchezaji halali wa
Yanga.
www.shaffihdauda.co: Sawa , Yanga ina washambuliaji kama
Ngoma, Busungu, Msuva, Kaseke, Tambwe, kufanya nao mazoezi kunakusaidiaje wewe
kama beki?
Juma Abdul: Yeah inanisaidia sana maana ukizungumzia
washambuliaji wa Yanga wote wapo vizuri kwa hiyo ukiwa kama beki unapaswa na
wewe kuwa vizuri sana ili uweze kuwakabili hao watu.
CHANZO: www.shaffihdauda.com
Post a Comment