Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba Madelu
kesho Jumamosi Mei 14,2016 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Ndanda na Young Africans katika mchezo
utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mbali ya Nchemba ambaye atakabidhi Kombe kwa Yanga ambao ni
mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2015/16, wageni wengi
maalumu watakaokuwa kwenye mchezo huo ni Mkurugenzi wa Vodacom, Ian Ferrao
sambamba na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pamoja na viongozi
wengine wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi ya Kuu Tanzania
Bara (TBLB).
Mchezo huo utafanyika kwa baraka za TPLB baada ya maombi ya
Young Africans kukubaliwa na Ndanda ambao watakuwa wenyeji wa mchezo huo utakaoanza
saa 10:00 jioni.
Mara baada ya mchezo huo, Mabingwa Young Africans watapewa
Kombe la ubingwa, medali na fedha Sh 81,345,723; Mshindi wa Pili Sh 40,672,861;
Mshindi wa Tatu Sh 29,052,044 na Mshindi wa Nne atazawadiwa Sh 23,241,635.
Mcehzaji Bora atapewa Sh 5,742,940 sawa na Mfungaji Bora wa
Ligi na Kipa bora wa michuano hiyo inayodhaminiwa na Vodacom,Bia ya
Kilimanjaro, Azam, Startimes na NHIF.
Mwamuzi Bora atazawadiwa Sh 8,614,610 sawa na Kocha Bora
wakati timu yenye nidhamu itavuna Sh 17,228,820.
Post a Comment