Mwanamme mmoja katika Mji wa Bungoma, Magharibi mwa Kenya
ameshangaza ulimwengu baada ya kudandia helikopta ambayo ilipaa angani na
kuondoka naye jana.
Helikopta hiyo ilikuwa imesafirisha mwili wa mfanyabiashara
mashuhuri nchini humo, Jacob Juma aliyeuawa kwa kupigwa risasi na kufariki
dunia jijini Nairobi wiki iliyopita, vyombo vya habari nchini Kenya vinasema.
Mfanyabiashara Jacob Juma, ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa
Kampuni ya Erad amekuwa akizua mjadala
mitandaoni Kenya kutokana na ujumbe wake anaoandika hasa kwenye Twitter,
aliuawa kwa kupigwa risasi jijini Nairobi wiki iliyopita.
Video zinazosambaa mitandaoni zinaonesha helikopta hiyo
ikipaa juu angani kutoka uwanja wa Posta, mwanamume huyo akiwa amejishikilia
kwenye vyuma vya helikopta hiyo.
Taarifa zinasema baadaye ndege ilitua kwa dharura katika
uwanja wa ndege wa Bungoma na mwanamume huyo kupelekwa hospitali.
Wengi wameeleza kushangazwa kwao na tukio hilo la aina yake
huku wengine baadhi ya Wakenya waliokuwepo kwenye tukio hilo, kwa imani zao
wakidai kuwa mwanamume huyo alisahau kama jana ilikuwa Ijumaa tarehe 13, ambayo
huwa ni siku yenye matukio mabaya.
Post a Comment