MAJIRANI Manchester United na Manchester City zipo vitani kumuwania kiungo mshambuliaji wa Schalke 04 ya Ujerumani, Leroy Sane mwenye thamani ya pauni milioni 40 sawa na Sh bilioni 125.5. Taarifa kutoka Man United na Man City zinasema klabu hizo zinapigana vikumbo kuhakikisha zinamnasa kinda huyo mwenye umri wa miaka 20 ili kuvipa nguvu vikosi vyao msimu ujao.



Sane japokuwa amezaliwa Ujerumani, ni mtoto wa straika wa zamani wa Senegal, Souleyman Sane aliyezaa na mama yake ni mwanamichezo wa sarakasi aliyewahi kutwaa medali ya dhahabu ya Olimpiki, Regina Weber. Kwa muda tofauti, klabu zote mbili zinaelezwa kutuma wawakilishi wake kujaribu kumsajili Sane ambaye amefanya vizuri katika timu yake msimu uliopita hivyo kuzivutia klabu hizo. Msimu huu, Sane ameichezea Schalke mechi 42 na kufunga mabao tisa huku akionyeshwa kadi za njano tano. Man City na Man United zinataka kuongeza nguvu ya ushambuliaji kwenye vikosi vyao msimu ujao baada ya kuteteleka katika Ligi Kuu England msimu huu na kuiacha Leicester City ikitwaa ubingwa.

Post a Comment

 
Top