LICHA ya
kutwaa ubingwa Jumapili iliyopita, kikosi cha Yanga kimeendelea kutoa dozi tena
leo mbele ya wenyeji Mbeya City baada ya kuibabua mabao 2-0 katika mchezo wa
ligi kuu uliofanyika katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Alikuwa ni
beki Vincent Bossou ambaye aliipatia Yanga bao la kwanza dakika ya 15 akiunga krosi iliyopigwa
na Juma Abdul ikitokana na kona fupi iliyopigwa na Simon Msuva.
Baada ya
kuona Yanga inatawa mpira, mashabiki wa Mbeya City walianza kurusha chupa na
mawe uwanjani kwa madai ya kutokubaliana na mamuzi ya mwamuzi baada ya
mshambuliaji Donald Ngoma kuonekana amejiangusha na refa kuonesha faulo
kuelekea upande wao.
Huku wengi
wakidhani matokeo yatabaki kuwa bao 1-0, mshambuliaji Amissi Tambwe aliipatia
Yanga bao la pili dakika ya 85 na kufikisha 21 baada ya kuachia shuti kali nje
ya 18 na kumshinda kipa wa City, Juma Kaseja.
Post a Comment