Ariana Yohana
VIONGOZI wa Kaizer Chiefs timu inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini wamegoma kuthibitisha ikiwa mshambuliaji hatari wa Simba Sports ya Dar es Salaam Ibrahim Ajibu anayetarajia kufanya majaribio klabuni hapo.
Haya yanakuja siku chache baada ya Ajibu kuondoka klabuni kwake bila kuaga kwa waajili wake.
Msemaji wa Klabu hiyo Vina Maphosa amedai Kaizer Chiefs haijatoa na haitatoa taarifa yoyote kuhusiana na mchezaji huyo ambaye wanajua  ameiudhi klabu yake ya Simba kwani ameondoka bila ruhusa, hadi hapo dirisha la usajili litakapofunguliwa.
"Siwezi kuzungumzia hilo kwa sasa, ila  ni kawaida yetu kama timu ikiwa kuna usajili unafanyika huwa tunawapa taarifa kupitia vyombo vya habari," aliuambia Mtandao wa Kickoff.com
Taarifa zinadai straika huyo amepewa siku kumi za majaribio klabuni hapo kabla ya kurejea Septemba ikiwa atafuzu majaribio hayo.
Imendikwa na Ariana Yohana na mtandao.

Post a Comment

 
Top