KOCHA wa Arsenal,
Arsene Wenger ameibuka na kusema uwepo wake katika kilabu hiyo uliisaidia timu
hiyo kupata mkopo wa ujenzi wa Uwanja wa Emirates ambao ndiyo uwanja wa
nyumbani wa timu hiyo.
Mashabiki
wanatarajiwa kufanya maandamano wiki hii baada ya kukasirishwa na matokeo ya
klabu hiyo msimu huu ambayo yamesababisha timu hiyo kushindwa kushinda taji la
ligi.
''Kipindi
tulipokuwa tunajenga Uwanja wa Emirates, benki zilitaka niweke sahihi ya mkataba
wa miaka mitano,” alisema Wenger, 66. ''Wataka kujua ni kilabu ngapi nilikataa
wito wao wakati huo?”
Ujenzi wa
uwanja huo uliogharimu pauni milioni 390 na ulianza mwaka 2004, mwaka ambapo
Wenger alishinda taji lake la mwisho la ligi na klabu hiyo.
''Benki
zilitaka niendelee kuwepo hapa ili wawe na uhakika ya kulipwa fedha zao,”
alisema wenger ambaye amekuwa akikinoa kikosi hicho tangu mwaka 1996.
Post a Comment