KOCHA
wa timu ya Taifa ya England, Roy Hodgson ametoa neno ambalo ni kama
anamhakikishia mshambuliaji wa Leicester City, Jamie Vardy kuwa atakuwemo
katika kikosi cha taifa hilo kitakachoshiriki michuano ya Euro 2016, Juni, mwaka
huu.
Kocha
huyo alitakiwa kutangaza majina hayo juzi lakini alisitisha na sasa atatangaza
kikosi chake keshokutwa Jumatatu, ili kupisha Premier League imalizike.
Hodgson
ametoa kauli hiyo wakati wa utoaji wa Tuzo za Mchezaji Bora wa England (FWA)
ambapo Vardy alikuwa mshindi.
Kocha
huyo alisema anajivunia kuwa na wachezaji wenye vipaji vya juu hasa katika
ushambuliaji ambapo aliwataja Jamie na Harry Kane kutokana na kasi yao ya
ufungaji msimu huu.
Mwaka
huu umekuwa mzuri hasa kwa washambuliaj, wamefanya kazi nzuri, nitatangaza
majina ya wachezaji 23 ambao watasafiri kwenda Ufaransa kuiwakilisha nchi
katika Euro 2016.
“Nampongeza
Vardy kwa kushinda tuzo na alistahili kuipata, sitakuwepo kwenye tuzo lakini
nawatakia jioni njema na mafanikio mema wote,” alisema Hodgson ambaye hakuwepo
katika tuzo hizo bali hotuba yake ilisomwa na mtu mwingine.
Post a Comment