Na
Ariana Yohana
ATLETICO Madrid imeripotiwa kuwa imepandisha dau la
mshambuliaji wake Antoine Griezmann na sasa kuwa pauni milioni 79.
Manchester United na Chelsea zote zimetajwa
zinamuwania vikali nyota huyo. Atletico imesema kuwa itakuwa tayari kumuachia
mpachika mabao wao huyo kwa timu yoyote itakayotoa kiasi hicho cha fedha.
Inaaminika kuwa Atletico watakuwa tayari kupokea
dau la si chini ya pauni milioni 63 lakini taarifa zilizotoka leo kwenye Daily
Mail zinadai Atletico imepandisha dau la usajili na kuwa pauni milioni 79.
Straika huyo ambaye aliisaidia Atletico kutinga
fainali ya UEFA, amekuwa akitajwa mara kwa mara kutakiwa na klabu hizo za
Uingereza kwa ajili ya kuungana na mojawapo tayari kwa kufanya nayo kazi msimu
ujao.
Post a Comment