Klabu ya soka ya Atletico Madrid imefanikiwa kutinga fainali
ya klabu bingwa barani Ulaya kwa mara ya pili ndani ya kipindi cha miaka mitatu
baada ya kupata bao la ugenini walipokipiga dhidi ya Bayern Munchen ya
Ujerumani.
Wakiwa na faida ya bao la nyumbani katika nusu fainali ya kwanza
nchini Hispania, Bayern walisawazisha kupitia mkwaju wa adhabu ndogo uliopigwa
na Xabi Alonso.
Mlinda mlango wa Atletico Jan Oblak aliokoa mkwaju wa
penalti uliopigwa na Thomas Muller kabla ya mshambuliaji Antoine Griezmann
kusawazisha na kuwa 1-1
Kipa wa Atletico akiokoa penalti
Robert Lewandowski alifunga bao la pili baada ya kupokea
pasi ya mpira wa kichwa kutoka kwa Arturo Vidal huku Atletico wakishindwa
kusawazisha baada ya mkwaju wa penalti uliopigwa na Fernando Torres kuokolewa
na mlinda mlango Manuel Neuer.
Kwa maana hiyo Atletico watakutana katika fainali mjini
Milan tarehe 28 Mei na mshindi wa mchezo kati ya Real Madrid na Manchester City
utakaopigwa kesho dimbani Santiago Bernabeu.
Post a Comment