KIUNGO wa
Arsenal na Timu ya Taifa ya England, Oxlade-Chamberlain ataikosa michuano ya
Kombe la Ulaya ‘Euro 2016’ kutokana na kuwa majeruhi wa goti.
Michuano ya Euro
inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 10, mwaka huu. England ipo Kundi B ikiwa
na Urusi, Slovakia na Wales.
Staa huyo
alikuwa na tatizo hilo kwa muda mrefu lakini akiwa anaelekea kupona alijikuta
akijitonesha Jumatatu iliyopita na tayari Kocha Arsene Wenger amethibitisha
kuwa atakuwa nje kwa wiki kati ya sita hadi nane, hii inamaana kuwa sasa
atarejea msimu ujao.
Mara ya
mwisho kucheza ilikuwa katika mchezo dhidi ya Barcelona kwenye Ligi ya Mabingwa
Ulaya uliopigwa Februari 23, mwaka huu na mpaka sasa amecheza mechi 33 katika
michuano yote akiwa na kikosi cha Arsenal.
Wenger
alisema: “Hana nafasi kwenye michuano ya Euro. Atarejea mwanzoni mwa mwezi Julai
mwaka huu.”
Post a Comment