KOCHA
wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho amethibitisha kuwa mipango yake ni kurejea
kwenye kazi ya ukocha rasmi Juni 30, ambapo ndipo atasaini mkataba mpya.
Mourinho,
53, amekuwa akihusishwa kujiunga na Manchester United hajasema kuwa ni klabu
ipi ambayo ataanza nayo kazi itakapofika siku husika licha ya kusema kuwa hajui
chochote kuhusu yeye kutua Man United.
Mourinho,
alifukuzwa kazi Chelsea, Desemba, mwaka jana baada ya matokeo mabaya ya timu
hiyo, alikuwa nchini Mexico juzi kwa ajili ya mechi ya hisani iliyohusisha
mastaa wa zamani wa soka kwenye Uwanja wa Azteca, Mexico City.
Alipoulizwa
juu ya kuwa nje ya kazi ya ukocha muda mrefu alisema: “Bila shaka nimemisi sana
kazi ya ukocha, itakapofika mwisho wa mwezi Juni nitakuwa nimesharejea, leo ni
Mei, naendelea kufurahia maisha, nafurahia na familia yangu lakini amini kuwa
Julai nitakuwa kazini.”
Alipoulizwa
lini hasa atasaini mkataba mpya wa kazi yake hiyo alijibu: “Juni 30, ndiyo siku
husika.”
Post a Comment