BEKI mkongwe wa Liverpool, Kolo Toure amemwambia beki
mwenzake kikosini hapo, Mamadou Sakho kuwa anatakiwa kuwa imara na mvumilivu
wakati huu ambao anakabiliwa na skendo yake ya kutumia dawa za kuongeza nguvu
mchezoni.
Mpaka sasa Sakho amefungiwa siku 30 wakati uchunguzi zaidi
ukiendelea juu ya sakata lake hilo, ambapo atakosa mechi zote zilizosalia
katika Ligi Kuu ya England ‘Premier League’.
Toure amesema hayo kutokana na kile kilichowahi kumkuta mwaka
2011 ambapo alitumia dawa zinazofanana na hizo za Sakho zilizomuingiza
matatizoni, ambapo alifungiwa kucheza soka kwa miezi sita.
SAKHO NA KOPP
“Najua ana bahati kwa kuwa niko hapa kumsaidia, nawasaidia
wachezaji wadogo zangu kwa ushauri hata kwa kupitia makosa yaleyale ambayo
niliyafanya mimi,” alisema Toure.
“Anachotakiwa ni kuwa mvumilivu, kuendelea kupambana wakati
huu mgumu kutokana na makosa aliyoyafanya.
“Hata mimi nilipokuwa Arsenal nilijifunza mengi kutoka kwa
walionizidi, nilijifunza kutoka kwa Martin Keown.
“Nilipopata tatizo hilo nilikuwa na fikra chanya, ndiyo maana
niliendelea kucheza.”
Post a Comment