WACHEZAJI WA ENGLAND WAKISHANGILIA |
MSHAMBULIAJI wa zamani wa England, Alan
Shearer amesema kuwa anashauri washambuliaji Jamie Vardy na Daniel Sturridge waanze
katika mchezo ujao kwenye michuano ya Euro 2016 inayoendelea nchini Ufaransa.
Harry Kane ndiye aliyekuwa chaguo la kwanza
katika mechi zote mbili ambazo England imecheza katika michuano hiyo lakini
ameshindwa kuwa na makali huku Vardy na Sturridge wakionyesha makali muda mfupi
baada ya kuingia katika mechi ya juzi dhidi ya Wales.
Shearer amesema unapokuwa straika unatakiwa
kuwa na makali na tayari muda wote, ukipata nafasi na ukashindwa kuitumia
vizuri utakosolewa na watu wengi wakiwemo wachambuzi kama mimi.
SHEARER |
Mkongwe huyo amenukuliwa akisema: “Unapokuwa
katika michuano kama hiyo ni jambo gumu kwa kuwa ndani ya mwezi mmoja unatakiwa
kuthibitisha ubora wako, kwa mabao aliyofunga Kane akiwa Tottenham tulitegemea
kuwa angekuwa na faida katika mechi mbili za Euro lakini imekuwa tofauti.
“Hata sisi ilitutokea katika Euro 1996 na
tulipata wakati mgumu, presha ilikuwa juu. Kwa kuwa Kane hakufunga katika mechi
mbili basi ni vizuri kuwatumia Sturridge na Vardy.
“Safu ya ushambuliaji ya England haikuwapa
wakati mgumu mabeki wa Wales hasa kipindi cha kwanza na pia hazikutengenezwa
nafasi nyingi.”
Post a Comment