KUNA
uwezekano mkubwa beki mpya wa Yanga, Andrew Vincent ‘Dante’ akachezeshwa kesho
Jumapili dhidi ya MO Bejaia ya Algeria, mwenyewe amesema akipata nafasi hiyo
hatatoka kikosi cha kwanza.
Yanga kesho Jumapili inatarajiwa kucheza na MO
Bejaia mechi ya Kundi A ya Kombe la Shirikisho Afrika kwenye Uwanja wa l’Unite
Maghrebine uliopo Bejaia, Algeria.
Dante aliyesajiliwa na Yanga siku chache
zilizopita kutoka Mtibwa Sugar, ana nafasi kubwa ya kucheza katika beki ya kati
na Kelvin Yondani kwani Nadir Haroub ‘Cannavaro’ hayupo kikosini.
Cannavaro anatumikia adhabu ya kadi nyekundu
aliyoipata dhidi ya Sagrada Esperanca na Vincent Bossou ambaye hucheza nafasi
hiyo, naye hakufanya mazoezi kikamilifu na wenzake kutokana na kuchelewa
kujiunga nao.
Akizungumza kutoka Algeria, Dante alisema: “Kwa jinsi nilivyo fiti kutokana na mazoezi
niliyofanya kambini Uturuki, naamini nikipata nafasi kikosi cha kwanza
sitatoka.”
“Nitacheza kwa juhudi kubwa kumvutia kocha ili
awe ananipa nafasi kila mara kikosini, labda nisipangwe lakini nikicheza tu
nitahakikisha sikai benchi .”
Dante anayemudu kucheza nafasi zote za ulinzi
na kiungo mkabaji, alisema kambi ya muda iliyoweka Yanga nchini Uturuki tangu
Jumapili iliyopita hadi jana Ijumaa, imewasaidia kwa kiasi kikubwa.
Mbali ya Dante, hadi sasa Yanga imewasajili
Hassan Kessy kutoka Simba, Juma Mahadhi (Coastal Union) na Beno Kakolanya
kutoka Prisons.
Post a Comment