Ariana Yohana na mtandao
KOCHA wa timu ya taifa ya Ireland, Martin O'Neill amesema kuwa amemshauri msaidizi wake, Roy Keane kunyoa ndevu kwa kuwa zinamfanya kuwa na mwonekano mbaya.

“Nilikuwa namwambia anyoe ndevu zake kwa kuwa wakati aliponikumbatia tukishangilia ushindi zilikuwa zikinichoma na sitaki anikumbatie tena,” alisema O'Neill, 44.

Makocha hao kwa pamoja wapo katika michuano ya Euro inayoendelea nchini Ufaransa ambapo alitoa kauli hiyo mara baada ya mechi ya mwisho hatua ya makundi dhidi ya Italia, walishinda na kufanikiwa kufuzu hatua ya mtoano.

Wakiwa katika hali ya furaha walikumbatiana na walionekana wakizungumza, jambo ambapo ndipo O'Neill alisimulia walichokuwa wakizungumza kuwa kilihusiana na ndevu za Keane.

“Nilikuwa namwambia anyoe ndevu zake kwa kuwa wakati aliponikumbatia tukishangilia ushindi zilikuwa zikinichoma na sitaki anikumbatie tena,” alisema O'Neill, 44.

Licha ya kujulikana kwa tabia yake ya kuwakosoa wachezaji na makocha bila kung’ata maneno, Keane ameendelea kuwa kipenzi cha O'Neill katika kazi ya ukocha na ameendelea kufanya naye kazi kwa muda.

Post a Comment

 
Top