Miaka iliyopita sneakers (raba) zilikuwa zinatumika zaidi kwenye kufanyia mazoezi. Mambo yamebadilika. Sneakers zinaweza kuvaliwa kwenye outfit na ukaonekana nadhifu. Wakati wa majira ya joto (kama hivi sasa kwa nchi za magharibi) utagundua kwamba sneakers zimekuwa miongoni mwa vitu vinavyovaliwa zaidi hususani kwenye mitoko ya kawaida. Wanawake nao wanashika hatamu siku hizi kwenye sneakers.
Kwa wale wanaotamani kutoka wakiwa simple but stylish unaweza kujaribu kuvaa outfit na sneaker. Wabunifu kama Giuseppe,Adidas, Converse wapo mstari wa mbele kutengeneza sneakers kwa ajili ya wanawake ambazo zinatumika kama vivazi nje ya mazoezi.
Unaweza kuvaa sneakers na aina nyingi za nguo kuanzia sketi,jeans,kaptula na hata magauni ya maxi. Hawa ni wachache walionifurahisha jinsi walivyovaa sneakers zao na outfits.
Post a Comment