KIPA na
nahodha wa Hispania Iker Casillas amesema hatastaafu mchezo wa soka mpaka pale
kipa na nahodha wa timu ya taifa ya Italia, Gianluigi Buffon atakaposema
imetosha yaani amestaafu.
Akiongea na Jarida
la Michezo la Italia la La Gazzetta Dello Sport, kutokea nchini Ufaransa alikokwenda kuitumikia Hispania katika
michuano ya Ulaya (Euro) Casillas,35, amesema haoni sababu ya kustaafu kwasasa
wakati wachezaji wenye umri mkubwa kuliko yeye kama swahiba wake,Gianluigi
Buffon bado wanatamba viwanjani.
Amesema
"Kuhusu kustaafu! Nadhani Buffon atakapostaafu,nitastaafu pia. Amesaini
mkataba mpya hivi karibuni na hilo litanifanya niwe na furaha kwa sababu nina
imani na mimi nitasaini pia.
"Muda
wetu wa kustaafu utakapofika,tutaandaa mchezo kati ya marafiki zangu na
marafiki zake kuhitimisha zama zetu"
Kauli hiyo
ya Casillas imekuja baada ya hivi karibuni Buffon,38, kusaini mkataba mpya wa
miaka miwili katika klabu yake ya Juventus.Mkataba huyo mpya utamfanya Buffon
aendelee kucheza soka la ushindani mpaka atakapofikisha umri wa miaka 40 hapo
mwaka 2018.
Kwasasa
Casillas anaichezea FC Porto ya Ureno na ana kipengele katika mkataba wake
kinachomruhusu kuendelea kucheza mpaka mwaka 2018.
Post a Comment