Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amempongeza Yussuf
Manji kwa kuchaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Young Africans SC baada ya kupata
kura 1,468 kati ya 1,470 zilizopigwa. Kura mbili ziliharibika kwa nafasi hiyo.
Kadhalika
Rais Jamal Malinzi amempongeza Clement Sanga kwa kuchaguliwa kuwa Makamu
Mwenyekiti baada ya kupata kura 1,428
wakati mpinzani wake Titus Osoro alipata kura 80. Kura 1,508 zilipigwa katika
nafasi ya kuwania makamu mwenyekiti.
Kadhalika
wajumbe wanane wanaounda Kamati ya Utendaji kwa kuchaguliwa kuongoza Klabu ya
Young Africans kwa miaka minne ijayo kwa mujibu wa katiba.
Wajumbe
waliochaguliwa ni Omary Said (1,069), Siza Lyimo (1,027), Salum Mkemi (894),
Thobius Lingalangala (889), Ayoub Nyenzi ((889), Samwel Lukumay (818), Hussein
Nyika (770) na Hashim Abdallah (727.
Katika
salamu hizo za pongezi, Rais Jamal Malinzi pia amewapongeza wanachama wa Young
Africans kwa kufanya uchaguzi wa amani na utulivu.
Kutokana na
hali hiyo, Rais Jamal Malinzi amewataka uongozi huo wa Young Africans kufungua
ukurasa mpya wa kuendesha klabu hiyo na kuiletea mafanikio klabu hiyo kongwe na
maarufu katika ukanda wa nchi za Afrika Mashariki na Kati hasa wakati huu
ambako Young
Africans
inashiriki hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC).
Post a Comment