Akizungumza mbele ya kipaza sauti cha kamera za East Africa Redio kupitia kipindi cha Planet Bongo, mkali wa R&B, Beka amesema ni ngumu kujiunga kwenye Lebo ya msanii Ali Kiba  na kwamba yeye tayari yupo kwenye uongozi, ambao unamsimamia kazi zake.
“Suala la kuwa tayari kusainishwa na Alikiba haiwezekani kwa sababu mi nipo kwenye management ambayo nina mkataba nayo, management ambayo imeninulia vifaa vya bendi, na sasa hivi ndani ya miezi hii mitatu au minne mbele nitazindua bendi yangu”, alisema Beka.
Pia Beka amesema yeye ameamua kuurudia Wimbo wa Aje wa msanii huyo kwa kuwa anaupenda na pia ni shabiki mkubwa wa Alikiba, hivyo ameamua kumpa ushirikiano msanii huyo.
“Kufanya ngoma ya Alikiba mimi ni shabiki wa Alikiba, naipenda na nyimbo ya Alikiba ndio maana nikaamua niimbe kwa feelings zangu lakini kutumia maneno yake, na pia napenda usapoti vya nyumbani kwa hiyo nikaona nimsapoti brother”, alisema Beka.

CHANZO: EA Radio

Post a Comment

 
Top