KIPA tegemeo hivi sasa wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiapiza kurejea jijini Dar es Salaam na pointi tatu wakati timu yake itakapovaana na MO Bejaia ya Algeria.
Yanga inatarajiwa kuvaana na MO Bejaia kwenye mechi ya 
Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kesho Jumapili
 huko Algeria.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Dida alisema maandalizi waliyoyafanya nchini Uturuki timu hiyo ilipoweka kambi yanatosha
 kabisa kupata ushindi kwenye mchezo huo.
Dida alisema: “Pia ubora wa kikosi chetu na umoja uliopo kwa 
wachezaji unatupa matumaini ya kufanya vizuri kwenye michuano 
hii migumu.”


Post a Comment

 
Top