Faraja Yohana
Klabu za Azam na Simba zinapigana vikumbo kuwania saini ya
mshambuliaji wa Tanzania Prisons Jeremiah Juma
Mshambuliaji huyo ameiambia Tanzaniabettingarena, bado
hajajua mustakabali wake wa siku zijazo kwakuwa bado ana mkataba na Prisons
aliyoichezea kwa mafanikio makubwa akifunga mabao 15.
“Nafurahi kuona timu kubwa za Azam na Simba zikinihitaji
lakini bado nina mkataba na timu yangu ya Prisons kama wananihitaji wazungumze
na uongozi wa timu yangu wakielewana nipo tayari kujiunga na timu yoyote kati
ya hizo mbili,”amesema Juma.
Juma ameonekana kufanya vizuri akiridhi kipaji alichokuwa
nacho baba yake Juma Mgunda ambaye alikuwa hodari katika kufunga mabao
akiichezea Coastal Union ya Tanga.
Add Facebook: Faraja
Yohana
Post a Comment