MADRID,
Hispania
HII
sasa vita, kwani baada ya Manchester United kutajiwa bei ya kiungo Paul Pogba
wa Juventus kuwa ni pauni milioni 95, Real Madrid nayo imeingia vitani
kumuwania nyota huyo.
Rais
wa Madrid, Florentino Perez hakuwahi kuwa shabiki mkubwa wa Pogba hata wakala
wa mchezaji huyo, Mino Raiola hivyo klabu hiyo haitaki kumuhusisha katika dili
hilo.
Lakini
taarifa za ndani ya Madrid zinasema, klabu hiyo inataka kumfanya Pogba kuwa
mchezaji wa kwanza kumsajili msimu huu licha ya upinzani uliopo kutoka timu za
Ligi Kuu England.
Licha
ya upinzani huo, lakini Madrid imepata nguvu baada ya Pogba kudaiwa kuchagua
kucheza Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’ kuliko kurudi England katika klabu yake ya
zamani Man United.
Kuna
uwezekano Madrid ikamtoa kiungo wake Isco kwenda Juventus ili kurahisisha
usajili wa Pogba ili kulainisha klabu hiyo ambayo ilikuwa ikimtaka mchezaji
huyo.
Wakati
huohuo, Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ameonyesha nia ya kumsajili kiungo wa
Leicester City, N'Golo Kante.
Kante
raia wa Ufaransa ana umri wa miaka 25, thamani yake inatajwa kuwa pauni milioni
20. Hata hivyo, Wenger ataingia katika vita na klabu za Chelsea na PSG
zinazomuwania kiungo huyo.
Katika
kuonyesha hisia zake kwa Kante, Wenger alisema: "Navutiwa na uchezaji wake
napenda wanaocheza kama N'Golo Kante.”
Post a Comment