DUNIA
ya wapenda soka, hasa Waafrika, bado inaomboleza kifo cha gwiji wa Nigeria,
Stephen Keshi, aliyefariki dunia Jumanne iliyopita kutokana na kile
kilichodaiwa kuwa ni shambulio la moyo.
Keshi,
amekwenda lakini huku nyuma ameacha rekodi mbalimbali ambazo zilimfanya
aonekane ni mtu wa kipekee. Kwanza, unatakiwa ujue kwamba Keshi, raia wa
Nigeria, ni kocha mweusi mwenye mafanikio zaidi kwa wakati wote.
Pia
Keshi, ni mmoja kati ya wanaume wawili tu waliowahi kutwaa taji la Kombe la
Mataifa ya Afrika kama mchezaji na kama kocha, lakini pia ni kocha wa kwanza
mweusi kutoka Afrika kufundisha katika hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia.
Timu yake ya kwanza kufundisha ilikuwa ni Togo. Hata
hivyo, kinachokumbukwa zaidi akiwa na timu hiyo ni pale alipotaka kupigana na
supastaa wa Togo, Emmanuel Adebayor kwenye Afcon 2006. Straika huyo hakupangwa
katika mchezo wa kwanza dhidi ya DR Congo, baadaye kwenye basi huku timu hiyo
ikiwa imefungwa 2-0, zilitokea vurugu kati ya Adebayor na Keshi ambaye
alionekana akizuiwa na wachezaji wa Togo asimvae straika huyo.
Mke wa Keshi aliyedumu naye kwa miaka 33, alifariki
dunia Desemba, mwaka jana. Dah! Wote wawili? Inauma sana
Post a Comment