Nahodha wa Argentina na mshambuliaji wa nchi hiyo na klabu ya Barcelona Lionel Messi ametangaza kustaafu kuchezea timu ya taifa.
Uamuzi huo umekuja masaa machache baada ya kukosa penati na kushindwa kuchukua kombe la mataifa ya America Maarufu kama Copa America Argentina ikifungwa kwa penati 4-2 na Chile.
"Kwangu mimi kuichezea timu ya taifa ndiyo mwisho sasa, Nimefanya kila nilichokiweza na inauma kuukosa ubingwa" Alisema Messi ambaye pia ni mchezaji bora wa dunia
Messi mwenye miaka 29 hivi sasa alikua akicheza mchezo wake wa 112 akiwa na Argentina tangu alipoanza kuitumikia nchi hiyo mwaka 2005.
Licha ya mataji mengi aliyoshinda Messi akiwa na Barcelona hajawahi kushinda taji lolote akiwa na timu yake ya taifa ukiacha medali ya gold ya michezo ya Olimpiki mwaka 2008 jijini Beijing.
Argentina wakiwa na Messi wamepoteza fainali 4 wakipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Ujerumani mwaka 2014, na fainali tatu za Copa America yani mwaka 2007,2015 na 2016.
Post a Comment