WAKATI nyota wa Ureno, Cristiano Ronaldo akisema nchi yake itatwaa ubingwa wa michuano ya Euro 2016, gwiji wa zamani wa Brazil, Pele, amesema, ni ngumu kwa timu hiyo kubeba taji.
Euro 2016 imeanza jana Ijumaa kwa wenyeji Ufaransa kucheza na Romania katika Kundi A, Ronaldo amesema huu ni wakati wao kwani kikosini wapo wazoefu kama Pepe na Luis Nani.
"Nadhani kwa kikosi cha sasa cha Ureno kinaweza kutwaa wa michuano mikubwa kama Euro na Kombe la Dunia, huu ni wakati wetu wa kuandika historia,” alisema Ronaldo.

Mwaka 2004 katika Euro, Ureno ilifungwa katika fainali kwenye ardhi yake ya nyumbani hivyo Ronaldo anataka sasa kupambana watwae ubingwa.
Hata hivyo, Pele ambaye ni gwiji wa zamani kwenye mchezo wa soka alisema: “Ni ngumu kwa Ronaldo na Ureno kutwaa ubingwa wa Euro kwani timu nyingi zina vikosi vikali tazama Ujerumani, Ufaransa na Hispania jinsi zilivyo.”
“Si kwamba Ronaldo ni mchezaji wa kawaida lakini tazama kikosini yupo na kina nani? Hata hivyo wanaweza kufika mbali lakini kuhusu ubingwa nina shaka.”

Post a Comment

 
Top