KUNA wasiwasi mkubwa umeibuka kuhusu Cristiano Ronaldo. Anakabiliwa na kashfa mpya.
Si kwamba ile ya kupingwa na Neymar anayedai kwamba jina lake halikustahili kwenye tatu bora ya wanaoshindania tuzo ya Ballon d'Or, bali anadaiwa kujihusisha na ushoga.
Supastaa huyo wa kimataifa wa Ureno amedaiwa kuwa na urafiki na bondia wa kiume wa Morocco, Badr Hari na hivyo kuzua utata mkubwa kutokana na kasi ya kukua kwa urafiki huo.
Imedaiwa kwamba nyota huyo wa Real Madrid mwenye umri wa miaka 30, mara kwa amekuwa akipanda ndege binafsi na kwenda Morocco kukutana na rafiki yake huyo.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari za Hispania, Ronaldo mara kwa mara amekuwa akienda Morocco kila baada ya mazoezi akitumia ndege yake binafsi aliyonunua kwa Pauni 14 milioni na hivyo kuzua utata mkubwa.Daniel Riolo  mchangiaji wa kipindi cha ‘Touche pas a mon sport’ kinachorushwa na televisheni moja ya Kifaransa alisikika akisema wawili hao, Ronaldo na Hari ni zaidi ya marafiki wa kawaida.
Kwa mujibu wa The Sun, Riolo alisema: “Ronaldo anakwenda Morocco mara tatu hadi nne kwa wiki kwenda kuonana na rafiki yake.Imedaiwa pia Ronaldo amefanya upasuaji wa kuremba pua yake. Kipindi hicho cha televisheni kinatangazwa na Estelle Denis kina mashabiki zaidi ya 400,000.
Ronaldo kwa siku za karibuni amekuwa akihusishwa na mpango wa kurejea Manchester United, alionekana akiwa kwenye picha mbalimbali na Hari.
Kuna wakati alionekana akiwa amebebwa na Hari na picha huyo kuandikiwa maelezo yaliyoanza kuibua utata.Picha nyingine alizopiga Ronaldo na rafiki yake huyo ilionekana wakiwa wamewasha mishumaa na kupata mlo kama ilivyo utamaduni wa Kimorocco, ambapo picha hiyo iliyokuwa imetumwa kwenye mtandao wa kijamii iliyokuwa na maelezo ya kutatanisha.
Ronaldo amehusishwa na kashfa hiyo licha ya jina lake kutajwa kwenye orodha ya warembo kadhaa katika maisha yake.
Ronaldo aliwahi kuwa na uhusiano wa miaka mitano na mrembo mkali kabisa, mwanamitindo wa Urusi, Irina Shayk, lakini wawili hao waliachana baada ya Irina kulalamika kwamba Ronaldo amekuwa akiwasiliana na marembo karibuni dunia nzima.
Tangu alipoachana na Irina, Ronaldo ameripotiwa kuwa na uhusiano na warembo Alessia Tedeschi na Maja Darving. Kipindi cha karibuni, Ronaldo ametajwa kutoka na mrembo, Marisa Mendes, binti wa wakala maarufu wa soka, Jorge Mendez.
Mwaka 2010, Ronaldo alidaiwa kusifia uamuzi wa Ureno kuruhusu ndoa za mashoga.
Ronaldo alisema: “Nikiwa kama Mreno, najaribu kutafuta ufahamu wa kila kitu kinatokea nchini kwangu.
“Lazima tuheshima chaguo la kila mtu, kwa sababu zaidi ya yote sote ni raia wenye haki na majukumu yaliyo sawa.”
Hata hivyo, Ronaldo hajazungumzia chochote kuhusu madai hayo yaliyoanza kuzagaa kutokana na picha zake alizopiga na bondia huyo wa ngumi za mateke wa Morocco.

Post a Comment

 
Top