KOCHA wa Sweden, Erik Hamren
amesisitiza kwamba, halitakuwa jambo jema kwa straika wake Zlatan Ibrahimovic
kuondoka kambini wakati huu na kwenda kukamilisha mipango ya kujiunga na
Manchester United.
Hamren alisema anafahamu kwamba,
usajili wa Ibrahimovic kwenda Man United upo katika hatua za mwisho lakini
halitakuwa jambo jema kwa sasa kwake kwenda England kusaini halafu kurudi tena
Ufaransa.
"Wachezaji wana ratiba ya
mapumziko katika kikosi changu, wanaweza kufanya lolote wakati huo na siwezi
kuwabana sana lakini haitakuwa vizuri kwa Ibrahimovic kutumia muda huo kwenda Manchester,"
alisema Hamren.
"Wachezaji wenzake wanajua jinsi
anavyokumbana na presha ya mambo ya usajili ila ni jambo la kawaida kwake na
ana uzoefu na mambo haya kwa muda mrefu.”
Sweden itaanza kampeni yake ya Euro
2016 katika Kundi E kwa kucheza na Jamhuri ya Ireland kabla ya kukutana na Italia
na Ubelgiji.
Post a Comment