KAIMU
Kocha Mkuu wa Simba, Mganda, Jackson
Mayanja, amewatoa hofu wanachama wa timu yake na kusema muda wowote atatua
nchini tayari kusimamia zoezi la usajili.
Mayanja, raia wa Uganda, alipewa likizo ya wiki
mbili huku akiwa na matatizo ya kifamilia, lakini sasa yameisha na akili yake
yote ipo kwenye mipango ya kuisuka upya timu yake.
Akizungumza na Championi Jumamosi kutoka
Uganda, Mayanja alisema anasubiri uongozi wa Simba umtumie tiketi ya ndege ili
arudi Tanzania kwa ajili ya kuanza maandalizi ya msimu ujao.
“Waliniambia watanitumia tiketi ya ndege ili
nirudi Tanzania kuanza maandalizi ya msimu ujao, mpaka sasa (jana) hawajatuma
ila nawasubiria wakituma tu nakuja.
“Nafahamu yanayoendelea, kila kitu kwenye ripoti
niliwaelekeza maeneo ya kufanyia usajili, hivyo naamini watayafanya yale
niliyoyaainisha kwenye ripoti yangu ya msimu mzima,” alisema Mayanja.
Licha ya Mayanja kutoa kauli hiyo, tayari Simba
imehusishwa na usajili wa mabeki Salum Kimenya na Nurdin Chona wa Prisons na
Rahim Juma wa African Sports.
CHANZO: CHAMPIONI
Post a Comment